
MWILI WA NDUGULILE KUWASILI LEO
Mwili wa aliyekua Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani(WHO) kanda ya Afrika ambaye pia ni Mbunge wa kigamboni DKT. FAUSTINE NDUGULILE utawasili leo saa 6:30 mchana katika uwanja wa kimataifa Julius Kambarage Nyerere,Dar es salaam ukitokea india kwa ndege ya shirika la ndege la Ethopia.
mwii unatokea india ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mapaka umaauti kumpata Novemba 27, 2024 (akiwa na umri 55), mwili utapokelewa na Naibu Spika MUSSA HASSANI ZUNGU akiambatana na Wajumbe wa Tume,Katibu wa bunge, wawakilishi wa serikali na wawakilishi wa chama
mwili wa marehemu kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya JWTZ, Lugalo. December 02 utaagwa katika viwanja vya Karimjee kisha December 03 mwili wa marehemu utaagwa katika viwanja vya mchava kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho.