
JAY Z,DIDDY WASHITAKIWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 13, MWAKA 2000.
Rapa wa Marekani Jay-Z amejibu kesi inayodai kuwa yeye, pamoja na Sean "Diddy" Combs, walimnywesha dawa za kulevya na kumbaka msichana wa miaka 13 kwenye sherehe mwaka 2000.
Mshtaki huyo ambaye jina lake halikujulikana anadai alivamiwa kwenye sherehe ya nyumbani baada ya Tuzo za Muziki za Video za MTV (VMAs) huko New York na kwamba mtu mashuhuri wa kike ambaye hakutajwa jina alikuwa kwenye chumba hicho wakati huo.
Katika taarifa yake, Jay-Z, ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter, alipuuza hatua hiyo ya kisheria na kusema ni "jaribio la ulaghai". P didy ambaye yuko jela akisubiri kesi yake baada ya kushtakiwa mwezi Septemba kwa biashara ya ngono na makosa mengine -alikanusha shtaka hilo.
Kesi hiyo iliwasilishwa mwezi Oktoba, na iliwasilishwa tena Jumapili ili kuorodhesha Bw Carter kama mshtakiwa.