
AJALI YA LORI UBUNGO RIVERSIDE
Mmoja anasadikiwa kufariki dunia na wengine Wanne kujeruhiwa, baada ya lori la mchanga lenye namba za usajili T405 DPJ kufeli breki na kugonga fremu tatu zinazouza samaki na magodoro eneo la Ubungo-Riverside, jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea mapema leo Jumatatu, Desemba 2, 2024 wameiambia LOKOLE APP kuwa gari hilo lilifeli breki wakati likishuka katika daraja la John Kijazi kuelekea Buguruni.